Alok Menon: 'Pengine maisha yangekuwa tofauti kama ningelinyoa nywele zangu mwilini, lakini kwanini iwe hivyo?'




Alok Menon
 
 
Alok Vaid-Menon ni mshairi na mwana harakati wa kutetea wanamitindo waliozaliwa na jinsia mbili (kiume na kike) katika mitandao ya kijamii. Lakini mara nyingi watu hukemjeli.
Mara ya kwanza alipoifahamisha familia yake kuwa ana jinsia mbili na kwamba angelipendelea kuangazia zaidi jinsia ya kike, swali la kwanza lilikua , "Lakini una nywele nyingi sana mwilini! Utapata tabu sana kuzitoa zote ili upate muonekano wa kike, kwa hivyo achana na wazo hilo."
Familia yake iliangazia zaidi nywele nyingi alizokuwa nazo mwilini kiasi cha kumzuia kujitambulisha kwa umma kama mwanamke

''Watu bado wana uelewa mdogioo kuhusu masuala ya watu waliyozaliwa na jinsia mbili'' alisema Alok Menon.
Jamii imetawaliwa na dhana ya kuwa watu waliozaliwa na jinsia mbili ima wanataka kuwa mwanamume au mwanamke lakini haijawahi kutathmini mahitaji mingine ya watu hao linapokuja suala la jinsi wao wanavyotaka kutambulisha jinsia yao kwa hadharani.
Alipoamua kuangazia jinsia yake ya kike zaidi japo muonekano wake ni wa kiume alijiunga na kikundi cha watu waliyozaliwa na jinsia mbili kama yeye ili kubadilishana mawazo na pia kupeana motisha kuhusu hali wanazokumbana nazo katika jamii.
''Nimekuwa nikibadilisha mavazi yangu kulingana na hisia zangu wakati mwingine navaa mavazi ya kiume na mara nyingine navalia mavai ya kike, hali hiyo ilikuwa ikiwakanganya watu sana'' alisema.
Kwa mfano akivalia rinda, wanawake walikuwa wakimchukulia kama mwanamke mwenzao na umuliza kwa mshangao "Alaa, sasa umekuwa mwenzetu?"

Share on Google Plus

About Mr PinkMoja@ TZ

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:

Chapisha Maoni

ANDIKA MAONI YAKO HAPA