DKT. MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA BANDARI DAR
Massawe akimkaribisha Dkt. MwakyembeWaziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wadau wa sekta ya bandari kwenye mkutano uliofanyika leo Jumanne Desemba 30, 2014 kwenye ofisi ya meneja wa bandari ya Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kutathmini huduma za
bandari na utekelezaji wa matokeo makubwa sasa kwa mwaka 2014. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Mwakyembe aliipongeza Mamlaka ya bandari kwa kazi nzuri ya utoaji huduma uliopelekea ongezeko la mizigo ingawa hata hivyo aliwajia juu wale wanaotia doa sifa nzuri ya bandari kwa kuendelea na tabia ya kunyanyasa wateja kwenye maeneo ya bandari kavu, na hata TRA. Aliagiza Mkuu wa TICST kuripoti ofisini kwake Jumatano saa mbili asubuhi akaeleze ni kwa nini amekuwa akitoza ushuru kwa kutumia viwango vya dola visivyo vya kiserikali. Pia alitoa wiki moja kwa kampuni ya AMI, kuhakikisha inalipa mzigo uliopotea wa mteja wake vinginevyo marufuko kufanya shughuli za kibandari. Mkutano huo ulikutanisha wafanyabiashara na watoa huduma ya usafirishaji wa makontena na mizigo inayopitia bandari ya Dar es Salaam, kutoka hapa nchini na DRC. Pia walihudhuria maafisa kutoka Bandari, TRA na SUMATRa
akizungumzakwa picha
fanyabiashara kutoka DRC John Kapeta, akizungumzaRais wa TAFAAfisa toka TRAMeneja
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA