Waziri
wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya
serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu.
Tarehe
hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo
Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni
maalum kwa ajili ya bajeti.
Ratiba
hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge
la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne,
ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa
Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25.
Mbali
na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada
kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali wa Mwaka, 2017
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA