Ikiwa
ni takribani miaka mitano tangu Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe,
avurugane na Chadema ambacho kilikuwa chama chake, sasa hali hiyo
inaonekana kurudi tena kupitia uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki
(EALA).
Tofauti
na awali ambapo alikosana na Chadema na kufukuzwa uanachama kutokana na
kile kilichodaiwa ni kuandaa waraka wa mabadiliko ya 2013, sasa hivi
ubunge wa EALA unaonekana kumvuruga tena mwanasiasa huyo na Chadema,
baada ya kuandika barua kwa Spika wa Bunge akitaka utaratibu
uliotangazwa wa namna ya kupata wabunge ubadilishwe.
Utaratibu
huo mpya uliotangazwa, unatoa nafasi kwa wabunge wa EALA kwa mwaka 2017
kulingana na idadi ya wabunge wa kila chama kwenye Bunge la Jamhuri ya
Muungano.
Kwa
mujibu wa Mwongozo huo, kutokana na idadi ya wabunge wa vyama kwa kila
chama, CCM imepata nafasi za wabunge sita kwenda EALA, Chadema mbili,
CUF moja, huku ACT Wazalendo pamoja na NCCR Mageuzi, vikiwa havina
nafasi hata moja kwenye Bunge hilo la Afrika Mashariki, kutokana na kuwa
na mbunge mmoja kila kimoja, hivyo kutokidhi vigezo.
Kutokana
na hali hiyo, Zitto ameliandikia Bunge barua kutaka Kamati ya Kanuni za
Bunge ikutane kujadili uchaguzi wa wajumbe wa Tanzania kwenye Bunge la
Afrika Mashariki.
Barua
hiyo, ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai inalenga kutaka
utaratibu wa awali ubadilishwe ili chama cha Zitto (ACT Wazalendo),
kimwingize mwanachama wake, Profesa Kitila Mkumbo kugombea ubunge huo,
inasema mwongozo uliotolewa na Bunge umekwenda kinyume cha Mkataba wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanasema
endapo hoja ya Zitto ikikubaliwa, ni rahisi zaidi wagombea wa Chadema
wakakosa nafasi hizo na badala yake nafasi za upinzani kuiwakilisha
Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki zikachukuliwa na wagombea wa
ACT na wale wa CUF.
Hali
hiyo inaelezwa kuchangiwa na wabunge wengi kwenye Bunge la Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania kuwa ni wa CCM, hivyo ni rahisi kuweka msimamo wa
kuwapigia kura wale wagombea wa ACT Wazalendo na wale wa CUF, badala ya
wale wa Chadema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.
Barua
ya Zitto ya Machi 28 iliyoandikwa kutokana na Tangazo la Bunge kwenye
gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti
yake, ilisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na
kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na siyo uchaguzi.
Alisema
pia mwongozo huo, mbali na kuvunja Mkataba wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, unataka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda
kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo.
Baada
ya Zitto kuandika malalamiko hayo, Mwanasheria wa Chadema, John Malya,
naye aliyajibu akirejea hukumu mbili za kesi ya Anthon Komu (kwenye
Divisheni ya Mwanzo na Divisheni ya Rufani).
Malya
aliandika kwamba, mwongozo wa Ofisi ya Spika wa Bunge wa kugawa idadi
ya viti kwa vyama ni sahihi, kwa sababu Divisheni zote mbili za Mahakama
ya Haki ya Afrika Mashariki ziliamua.
Katika
sehemu ya barua yake, alisema: “Mwenye kupaswa kubeba mzigo wa makundi
ya Zanzibar, Bara na Wanawake (ukiachilia mbali kundi la vyama vya
upinzani) ni chama chenye wabunge wengi (CCM)”.
Hoja
hiyo ya Malya inachambuliwa na Ado Shaibu, ambaye aliandika ujumbe
unaogusa hoja za kisheria ambazo alitumia Malya kukosoa malalamiko ya
Zitto.
Shaibu
alisema ni kosa kutumia kesi ya Antony Komu ambayo iliamuliwa na
Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama ya Afrika Mashariki, lakini baadaye
Divisheni ya Rufani ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ikatengua
hukumu hiyo kwa hoja ya kwamba Divisheni ya Mwanzo ya Mahakama haikuwa
na mamlaka ya kuamua suala husika.mr pinkmoja.com
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA