Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, ametoa siku saba kwa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kuhakikisha
linaanza zoezi la kuwarejesha Burundi wakimbizi walio tayari kurejea
nchini kwao.
Waziri
Nchemba ametoa agizo hilo leo Alhamisi Agosti 24, baada ya kutembelea
kambi za Nduta Wilaya ya Kibondo na Mtendeli wilayani Kakonko katika
ziara maalumu.
Nchemba
amesema iwapo siku saba zitafika kabla ya kuanza kwa zoezi hilo,
serikali itatumia magari ya jeshi kuwarejesha kwao kwakuwa wamekubal
wenyewe.
Kwa
mujibu wa mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma, Tony Laizer amesema
hadi sasa Kambi ya Nduta imesajili wakimbizi 8,743 ambao wameridhia
kurejea nchini kwao kwa hiari.
Mkuu
wa makazi katika kambi ya Nduta, Peter Bulugu, amesema hali ya usalama
si shwari maeneo ya kambi na nje ya kambi kutokana na baadhi ya
wakimbizi kujihusisha na wizi na uvamizi unaotokana na ukosefu wa
chakula cha kutosha na kushinikiza kurejeshwa kwao.
Kwa
upande wa Mwakilishi wa shirika hilo ofisi ndogo wilayani kibondo, Barb
Wigley ameiomba serikali kuwavumilia UNHCR kwakuwa vikao baina ya pande
tatu yaani serikali ya Tanzania, Burundi na UHNCR vinaendelea ili
kuwarejesha watu hao kwa staha.
Nchemba amesema msimamo wa serikali ni kuanza kuwarejesha wakimbizi hao katika muda uliopangwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA