Mbunge
wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi amefunguka na kusema ameagizwa na Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwaambia wana Mbeya pamoja na
Watanzania kiujumla kuwa wajiandae.
Joseph
Mbilinyi amesema hayo baada ya kumtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi
nchini Kenya na kusema kutokana na uimara ambao Tundu Lissu anao
amewataka Watanzania kujianda.
"Nimemtembelea
'Big hommie', Nairobi hospital. Ameniambia nikawaambie wana Mbeya kuwa
alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na
kuwa mwili wake 'uliovunjwa vunjwa' kwa risasi unazidi kuimarika na
atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana Mbeya na Watanzania wote
wajiandae, wajiandae, wajiandae" alisema Sugu.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi pamoja na Mbunge wa Iringa
Mjini juzi walimtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi Kenya anapopatiwa
matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa
nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7, 2017.
mr.pinkmoja/
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA