Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo November 1, 2017 imeelezwa kuwa jalada la
kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo ya Tsh. Milioni
785 inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa
Magufuli’ linaandaliwa kupelekwa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi kwenye ‘Mahakama ya Mafisadi’
Haya
yameelezwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
ulishakamilika na kinachofanyika sasa ni jalada la kesi hiyo kuandaliwa
ili liende Mahakama ya Mafisadi.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi November 15,
2017 ambapo katika kesi hiyo mbali ya Mpemba, Washtakiwa wengine katika
kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa,
mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo,
dereva na Pius Kulagwa.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh 785.6 milioni.
Inadaiwa
katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na October, 2015 wakiwa Dar
es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa
ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande vya
meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh
392.8 milioni bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
October
26, 2015 Washtakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya
meno ya tembo 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya dola za
Marekani 30,000 sawa na Sh 65.4milioni.
Wanadaiwa
kuwa October 27, 2015 wakiwa Tabata Kisukuru pia walikutwa na vipande
vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola
za Marekani 15,000 sawa na Sh 32.7 milioni.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA