Uongozi
wa kata ya Nyehunge wilayani Sengerema umepitisha sheria ya kuwacharaza
viboko 12 au faini ya Sh10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na
wanafunzi wa kike.
Sheria
hiyo ndogo imepitishwa juzi kwenye kikao cha maendeleo ya kata (WODC)
baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja
uzito kuzidi kuwa sugu.
Ofisa
mtendaji wa Kata ya Nyehunge, Mabula Enock alisema sheria hiyo
itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya
nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.
“Tumelazimika
kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel
Kipole aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi
wacharazwe viboko au kutozwa faini ya Sh10, 000 ama vyote kwa pamoja,”
alisema Enock.
Agizo
la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba mwaka 2017 wakati akikaribisha
wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya
Sekondari ya Nyehunge.
Diwani
wa kata hiyo, Charles Mbogo alisema kitendo cha kukatiza masomo si cha
kuungwa mkono, hivyo adhabu inapaswa kuongezwa na kuitaka jamii kuachana
na suala hilo.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisa elimu ya sekondari wa Buchosa,
Benjamini Siperato halmashauri hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,136 katika
shule 20 za sekondari 20 na mwaka 2016/17 wanafunzi 18 wa kike walipata
ujauzito, hivyo jamii inapaswa kuacha tabia ya kuwarubuni watoto wa
kike.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA