Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anatafakari uwezekano wa kuanza tena kuwanyonga wahalifu nchini humo.
Rais
Museveni amesema licha ya kwamba yeye ni "Mkristo" kuwa dini yake
imemzuia kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wale ambao wamehukumiwa
kunyongwa, hata hivyo amesema, hali hiyo imekuwa ikiwatia moyo wahalifu.
Kiongozi
huyo ametoa kauli hiyo wakati wa sherehe za kuhitimu kwa askari wa
idara ya magereza, katika gereza la Luzira jijini Kampala ambapo ni
miaka 13 sasa tangu Uganda ilipotekeleza hukumu ya kifo dhidi ya
wahalifu.
Watetezi wa haki za kibinadamu wameshutumu tamko hilo la Rais Museveni na kusema adhabu ya kifo haikomeshi uhalifu.
Mara
ya mwisho kwa Rais Museveni kuidhinisha hukumu ya kifo itekelezwe
ilikuwa katika gereza la Luzira mwaka 1999 na mwaka 2005 aliidhinisha
mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya kifo
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA