Magufuli ambadilikia Waziri na Mwanasheria Mkuu


 

Rais  Dkt. Magufuli leo Februari 1, 2018 amewabadilikia Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo ya msingi.

Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria na kusema yeye ameubwa kusema ukweli hivyo ataendelea kuusema hata kama kuna watu unawaumiza

"Kinachoshangaza pamoja na hatua nzuri ya Serikali kupeleka 'Legal Aid Act' ya mwaka 2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini 'regulation' mpaka saizi hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo 
"Jamani mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa, kwa hiyo wewe Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna 'Instrument' za kuweza kutoa uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini regulations mpaka leo miezi tisa imepita.

"Watu wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania.
" Ndiyo maana nawaambia changamoto zingine zipo ndani ya Serikali lazima na mimi nijitathimini ninachaguaagaje hawa watu ambao wanachelewesha chelewesha, hiyo ndiyo tathimini ambayo ninaanza kujifanyia kuanzia leo" alisema Rais Magufuli

Share on Google Plus

About Mr PinkMoja@ TZ

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:

Chapisha Maoni

ANDIKA MAONI YAKO HAPA