Timu nne za kundi C katika kombe la Afcon zitakuwa na ari tofauti nchini Misri mwezi huu huku Senegal na Algeria zikipigiwa upatu kusonga mbele katika kundi hilo nazo Kenya na Tanzania zikitajwa kuwa timu ndogo zinazoinuka.
Timu ya Algeria ilishinda taji hilo 1990 wakati walipokuwa wenyeji wa michuano hiyo ambapo wakati huo ni timu nane pekee zilizoshiriki huku Senegal ikikaribia kushinda taji hilo 2002 baada ya kulazwa kwa njia ya mikwaju ya penalti na Cameroon katika fainali.
Timu zote zinajigamba kumiliki nyota wa Ligi ya Uingereza akiwemo Sadio Mane wa Liverpool na Riyad Mahrez kutoka mabingwa wa ligi Man City ya Uingereza ambaye ni kiungo muhimu wa Algeria.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA