Na Amiri kilagalila-Njombe
Mahakama
ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe imemhukumu kifungo cha maisha
jela mtuhumiwa Addo Aron Nziku baada ya kukutwa na hatia ya kubaka
mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 katika kijiji cha kitulila halmashauri
ya mji Njombe.
Shauri
namba 31 la mwaka 2019, ni kesi iliyomkabili mtuhumiwa Addo Aron Nziku
mwenye miaka 26 mbena na mkazi wa kijiji cha matola halmashauri ya mji
Njombe, dhidi ya Jamhuri.
Shauri
hili likiwa chini ya hakimu James na Mhanusi na Mwendesha mashataka wa
serikali Nura Manja ambae ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa anadaiwa
kumwingilia mwanafunzi huyo zaidi ya mara tatu kabla ya mtoto huyo
kumweleza bibi yake juu ya maswahibu yanayompata.
Mtuhumiwa
Addo Nziku anadaiwa kumwingilia kimwili mtoto huyo kwa zaidi ya mara
tatu katika eneo la mabanzi yaliyoko nyuma ya nyumba ya wazazi wa mtoto
huyo huku mara ya tatu akimuingilia katika eneo la kukata majani ya
mifugo ambako mtoto huyo alitumwa kwenda kusaka majani ya simbilisi siku
ya tarehe 26 mwezi wa kwanza.
Mahakama
imemtia hatiani mtuhumiwa baada ya kujiridhisha na ushaidi uliotolewa
kwa kumkuta na hatia ya kubaka kinyume na kifungu cha sheria namba 130
kifungu kidogo cha kwanza na cha pili E sambamba na kifungu namba 131
kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu namba 16 kama
ilivyofanyiawa marejeo mwka 2002.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA