Na Matias Canal, Wizara ya Katib na Sheria-Dodoma
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Geofrey Pinda amewahakikishia watanzania
kuwa Serikali haina Sheria Kandamizi hivyo Sheria zote zinazotumika
nchini zilitungwa na Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambalo halijawahi kutunga Sheria Kandamizi.
Amesema
kuwa Serikali kwa kuzingatia mahitaji ya wakati na watu wake, imekuwa
ikiwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya Sheria mbalimbali ili
kuziboresha Sheria hizo.
Akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum Mhe Zainab Katimba aliyetaka kufahamu Serikali ina
mpango gani wa kurekebisha baadhi ya sheria kandamizi kwa wanawake ili
ziendane na wakati, Mhe Pinda amesema kuwa Kutokana na wakati uliopo na
mahitaji ya sasa Serikali imeanzisha mchakato wa kuzipitia baadhi ya
sheria ili ziweze kufanyiwa marekebisho kuendana na wakati.
Amesema
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa muswada wa
mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Ndoa utakaowasilishwa Bungeni
ili kuiboresha, kwa lengo la kulinda makundi ya wanufaika na Sheria
hiyo.
Aidha, Serikali inaendelea na hatua
mbalimbali za kupitia Sheria ya Usimamizi wa Mirathi na Sheria za
Kimila. Hatua hizo zikikamilika, Muswada wa mapendekezo ya kuzirekebisha
sheria hizo utawasilishwa Bungeni, ili Wabunge wapate nafasi nzuri ya
kujadiliana na kuyapitisha marekebisho hayo.
Mhe
Pinda amesem akuwa Wizara ipo katika mabadiliko makubwa ya kuhakikisha
kunafanyika maboresho makubwa ya Sheria zetu ikiwemo kuzitafsiri kwa
Kiswahili lakini pia kuweka vipengele kwenye sheria hizo vya kutoa
hukumu kwa lugha ya Kiswahili jambo ambalo litaleta tija kubwa katika
ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu.
Hivyo amewaomba
wabunge kuunga mkono juhudi za Serikali katika eneo hilo kwa lengo la
kuimarisha utawala wa Sheria na upatikanaji wa haki nchini.
That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA