Matumizi
ya Madawa ya kulevya hapa nchini yanaongezeka kwa kasi sana. Huku
ikionekana wasanii ni moja kati ya waathirika wa kubwa wa
janga hili. Tumeona hivi karibuni rapa mkongwe Chidi Benz jinsi alivyothorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
janga hili. Tumeona hivi karibuni rapa mkongwe Chidi Benz jinsi alivyothorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Kupitia
mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi kwamba Ray C amerudi katika
matumizi ya madawa ya kulevya ingawa mara kadhaa amekuwa akikanusha
taarifa hizo.
Waswahili
wana msemo mashuhuri usemao ‘Lisemwalo lipo’ kwa nini asitajwe msanii
wengine, na mara nyingi wasanii wote ambao hutumia Madawa ya kulevya,
uanza kwa kukataa hadi pale akapozidiwa ndipo anaweka wazi. Tumeshuhudia
kwa Chidi Benz, Ray C, Q Chief na wengine.
Februari
mwaka huu, Ray C alikanusha vikali taarifa ya kwamba amerudi kwenye
matumizi ya madawa ya kulevya , “Hata siju moja sikawahi pata msaada
wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli tu ya kuja kwenye dawa kila
siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa
dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala
msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani it’s not easy but am a
fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi
kujaribu, napambana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma
na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu,” aliandika Ray C katika
instagram yake.
Lakini
kauli hiyo bado haiendani na maisha yake halisi ya sasa, kwani Ray C
bado anadaiwa kuoneka katika mitaa ya Mwananyala akiwa katika hali mbaya
licha ya kuwa huu ni mwaka (3) akitumia dosi ya Methadone.
Rais
mstaafu Jakaya Kikwete tayari alishafanya kazi kubwa ya kumsaidia Ray C
na kumfikisha hapa alipo sasa. Huu ni wakati wa wasanii wenzake kupokea
kijiti na kumsaidia, Vita ya kupambana na Madawa ya kulevya ni ya wote,
kila mmoja amwongoze aliyepotea njia na sio kuiachia serikali.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA