Wakati
mwanaye staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama yake mzazi,
Sanura Kassim ‘Sandra’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss
Lady’ na mwanaye Tiffah wakiteketeza kiasi cha
fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.
fedha kinachokadiriwa kufikia shilingi Mil.100 barani Ulaya walikokwenda kula bata, baba mzazi wa msanii huyo, Abdul Juma anadaiwa kushinda njaa kutokana na ugumu wa maisha, twende na Risasi Jumamosi.
Baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mzee Abdul Juma.
Diamond
na familia yake hiyo sambamba na madansa wake, waliondoka nchini
mwishoni mwa wiki iliyopita kwenda Frankfurt, Ujerumani ambapo pamoja na
kufanya ziara ya kimuziki katika nchi tofauti balani Ulaya, staa huyo
aliitumia ziara hiyo kuponda raha.
Staa
wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mzazi mwenzake, Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’ pamoja na mtoto wao Tiffah wakila ‘bata’ Ulaya.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo
makini kililiambia gazeti hili mapema wiki hii kuwa, baba Diamond kwa
sasa ana maisha magumu na mara nyingi amekuwa akishinda njaa huku baadhi
ya majirani wakimpa msaada hali inayowasababisha kushangaa baada ya
kusoma kwenye magazeti kwamba mwanaye huyo anatumbua fedha kibao na
familia yake, ndugu na marafiki huku mzazi wake huyo akiteseka.
“Jamani baba Diamond anateseka! Muoneeni huruma. Alikuja kwangu kuniomba elfu moja lakini bahati mbaya na mimi sikuwa nayo. Mara nyingi amekuwa akishinda njaa. Mbaya zaidi anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hana mtu wa kumpeleka hospitali. Njooni mumuone yupo hapa kwake anatia huruma,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kiukweli baba Diamond anasikitisha sana. Tunashindwa kujua tatizo liko wapi kati yake na mwanaye, maana kuna wakati huwa anamsaidia lakini wakati mwingine anampotezea.”
MAPAPARAZI WAMUIBUKIA
Baada
ya kuzipata habari hizo, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa baba
Diamond, Magomeni ya Kagera jijini Dar na kumkuta nje ya nyumba yake
akiwa ameshika tamaa huku akionesha hali ya kunyong’onyea kama mtu
aliyekata tamaa ya maisha.
HALI YAKE NI MBAYA
Akizungumza
na gazeti hili baada ya salamu, baba Diamond alieleza kwamba bado hali
yake ya miguu ni mbaya kwani anatembea kwa kuburuza laiti angekuwa kama
zamani angeweza kufanya shughuli ndogondogo za kujipatia kipato angalau
apate fedha kwa ajili ya kula hasa katika kipindi hiki ambacho hana
msaada.
“Niko hapa bado mambo siyo mazuri, miguu inanisumbua kama unavyoona. Nasikia mwanangu (Diamond) ana ziara nje ya nchi na juzi niliona mmeandika ameteketeza milioni 100 na familia yake, namsubiri akirudi huko naamini atanisaidia angalau fedha hata ya kwenda kwenye matibabu na kula kama ataamua maana alishawahi kuniahidi, hali yangu siyo shwari nabangaiza tu hapa,” alisema baba Diamond.
DIAMOND ASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond aliyeko Ujerumani kwa sasa ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema hana cha kuzungumza kwa sasa.
“No comment kwa sasa, subirini nikirudi tutaliongea hilo kwa kirefu,” alisema Diamond.
ALIOKWENDA NAO ULAYA
Katika
gazeti lenye udugu wa damu na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu
iliyopita, ukurasa wake wa mbele lilikuwa na kichwa kisemacho; DIAMOND
ATEKETEZA SH. MIL 100 ULAYA.
Katika
habari hiyo, Diamond aliandikwa kusafiri na ‘ujumbe’ mrefu wa idadi ya
watu 14 ambao wote walikuwa chini yake kwa malazi na chakula. Watu hao
ni Zari, mama yake mzazi, Tiffah (mwanaye), Romy Jons (DJ wake), Kifesi
(mpigapicha), Salam (meneja), mke wa meneja wake mwingine Batu Tale,
madansa wanne na dada mmoja ambaye ni ndugu wa Zari. Hao walikwea pipa
na kufikia Frankfurt, Ujerumani.
BABA DIAMOND AMEFIKAJE HAPA?
Baba
Diamond anadaiwa akiwa angali kijana, alitengana na mama Diamond akiwa
na mtoto huyo mdogo kwa miaka mingi bila kumpa huduma zozote kitu
ambacho kimemsukuma Diamond kuwa na chuki na ashindwe kumpa matunzo
mzazi wake huyo baada ya kupata mafanikio.
Hata
hivyo, mara kadhaa Diamond amekuwa akimsaidia fedha baba yake huyo
lakini si kwa asilimia mia moja kama anavyomtunza mama yake ambaye
anaonekana kula raha hususan kipindi hiki ambacho bwana mdogo huyo
kutoka Tandale, maisha yamemnyookea.
Tazama Video Hapa:
Chanzo:Risasi
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA