Baada ya kuzagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikidai beki wa
Yanga, Vicent Bossou hajalipwa mishahara ya miezi minne, Katibu mkuu wa
Yanga amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.
Siku chache baada ya mechi ya Yanga na Simba, ulisambaa ujumbe
unaodaiwa kuwa wa beki huyo ukionyesha kulalamika kwamba hajalipwa
mishahara ya miezi minne.
Jumatano hii Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amefunguka
kwa kudai kuwa sio kweli kwamba mchezaji huyo anadai mshahara wa miezi
minne.
“Bossou haidai Yanga SC mishahara ya miezi minne kama habari
zinavyotembea . Check za mishahara ya beki huyu kwa siku 10 mwezi wa 12
na January zilikwisha andaliwa na mtoa check amemueleza kuja kuchukua
lakini sielewi kwa nini hakuzifuata,” ilisema taarifa hiyo kutoka kwenye
mtandao wa klabu hiyo.
“Kabla ya mechi na Simba SC alifanya vizuri mazoezi lakini kwa
taarifa zilizopo aliondoka mazoezini bila ruksa ya mwalimu . Tunasubiri
ripoti ya mwalimu kwa ajili ya kuchukua hatua,” aliongeza Mkwasa.
Katibu mkuu huyo hivi karibuni alitoa taarifa ya kuwa klabu hiyo kwa sasa inatatizo la kiuchumi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA