Mwanasheria
MKuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki leo tarehe 24 Agosti
2017 amepata dhamana ya polisi na kuweza kuachiwa huru baada ya
kushiliwa na jeshi hilo kwa siku mbili,
Tundu
Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Polisi kwa masharti ya kuripoti kituo
cha polisi siku ya Jumatatu ya tarehe 28 Agosti 2017 wakati wowote
akiwa na muda.
Tundu
Lissu alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kusema
makosa za Rais John Pombe Magufuli hadharani pamoja na kosa la uchochezi
kufuatia matamka yako aliyoyatoa kuhusiana na kuzuiliwa kwa ndege mali
ya Tanzania Bombadier Q400 nchini Canada kutokana na amri ya mahakama.
Mbunge
Tundu Lissu amepata dhamana masaa machache baada ya Uongozi wa juu wa
Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) kulitaka jeshi la polisi kumuachia
Tundu Lissu na kumkamata Mbunge William Ngeleja ambaye alirudisha fedha
za Escrow
"Hatuwezi
tukaipata 87bn kwa kumuweka Tundu Lissu ndani au kwa kuwashutumu
Wapinzani au watu kadhaa waliyoyaibua hayo, Unamuacha Willia Ngeleja
amerudisha pesa za Escrow ni sawa amekiri kosa, mtu anayeeleza ukweli
nchi inapata hasara anakamatwa, ni zaidi ya siku 4 tangu tamko la Chama
litolewe hazijatoka hoja Serikalini zinazopinga kwa hoja na vielelezo
kama tulivyolieleza" alisema Katambi
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA