Waziri
wa maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigangwala amesema kuwa watoa huduma
mbalimbali za utalii watatakiwa kufuzu mtihani kabla ya kupewa leseni
mpya kuanzia Januari 2018 ambapo Serikali itaandaa utaratibu mpya katika
sekta hiyo.
Ambapo
alisema kuwa Wizara yake iko katika mchakato wa kuandaa mwongozo kwa
ajili ya makampuni ya utalii nchini pamoja na kufunga mashine maalumu
ambayo itadhibiti mapato yatokanayo na utalii.
Aliongeza
kuwa wizara yake itarekebisha mfumo wa watoa huduma katika sekta hiyo
ambao umekuwa ukilalamikiwa na wadau mbalimbalui hasa watoa huduma za
utalii wanaowashawishi watalii kutoka nchi mbalimbali za nje kuja
kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini.
Dk.
Kigangwala aliyasema hayo jana wakati alipokuwa anazungumza na
watumishi wa Shirika la hifadhi la Taifa (Tanapa)katika ziara yake ya
kutembelea ofisi mbalimbali za shirika hilo.
Alisema
lengo hasa lakuanzisha mchakato huo utakaoanza kutumika mapema mwakani
nikuweka vigezo vitakavyotolewa na Serikali kwa makampuni ili
kuhakikisha wanakuwa na wahudumu watakaothibitishwa na wizara yake na
kutoa cheti maalum kwa kila anaetoa huduma hiyo ya utalii.
Waziri
huyo alisema lengo nikuboresha huduma za utalii ili kuwezesha
upatikanaji bora wa huduma za utalii na mapato ambayo yanainua uchumi
kwani Tanzania sasa inashindana na nchi mbalimbali katika
kuvitangazavivutio vya utalii ili kuhakikisha watalii wenguwanakuja
zaidi nchini kwetu.
Pia
aliongeza kuwa watoa huduma za utalii wanapaswa kuzungumza vizuri
kutoka nchi mbalimbali ili waweze kuja lakini pia waangalie jinsi ya
kuboresha huduma za utalii ikiwemo mapatona mfumo huu mpya wa kukusanya
mapatio ua sekta ya utalii kuboreshwa kuongeza mapato kwa mfumo wa
kieletronik.
Aliongeza
kuwa maeneo wanayoweka mkazo zaidi ni ukusanyaji wa mapato hiyvyo
kutakuwa na dirisha moja litakalounganisha taasisi za utalii kujua
mapato yanayoingia nikiasi gani na mtalii anakaa nchini kwa muda gani na
hoteli ip na kujua mapato yamnayokusanywa kwa sekta ya utalii yanakuwa
kwa kiasi gani.
Kwa
upande wake Mkurugeni wa Tanapa Allan Kijazi alisema kuwa utaratibu huo
utakuiwa mzuri na kpia wako katika mchakato wa kufungua ofifi katika
mkoa wa dodoma ili kuweza kusogeza huduma mbalimbali zinazotoklewa
nashirika huilo ili kuboresha sekta ya utalii na kuongeza pato la nchi
kupitia sekta hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA