Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Ndg Humphrey Polepole amerusha jiwe
gizani kwa Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe kwamba anajua wakati
huu anapitia wakati mgumu sana ndani ya chama ndiyo maana anatapatapa
katika suala la makubaliano kati ya serikali na Kampuni ya Uchimbaji
madini ya Barrick.
Akifanya
mazungumzo ndani ya Ofisi yake na EATV, Polepole amesema kwamba kitendo
cha Mbunge huyo kitendo cha Mbunge huyo kwenda kuzungumza kwenye chombo
cha habari na kuuhadaa umma kwamba madini yataendelea kuwa madini ya
watu wa nje, yeye hana tatizo naye kwani anafahamu wazi kwamba chama
kinaenda kumfia hivyo watu wamuelewe..
"Naomba
mumuelewe huyu bwana, anapitia wakati mgumu. Chama kinamfia tumuelewe
sana. Watu wote wenye uelewa mpana walioshiriki katika kukianziasha
chama wote wameondoka na wameondoka kwa masikitiko ya kwamba chama
kimepoteza dira. Asubiri kuona matokeo ya maendeleo yanayoletwa na
serikali. Mfama maji haishi kutapatapa ni sehemu ya asili ya ubinadamu.
Namwambia asubiri kuona maendeleo yatakuja kutokana na makubaliano haya
makubwa" Polepole.
Aidha
Polepole amesema kwamba Zitto ameshiriki katika kutunga sheria tatu
ndani ya Bunge kuhusu madini kisha akaenda ulaya kusema kwamba madini
yatazidi kuchukuliwa na wageni ni kuuhadaa umma kwani katika sheria
waliyoitunga ilikuwa ni ya kutamka kwamba madini yaliyopo ardhini ni
mali ya watu wa Tanzania.
Ameongeza
pia Sheria ya pili Mh. Kabwe aliyoshiriki ni pamoja na ile ya Kuipa
Mamlaka Bunge kutazama masuala ya madini vizuri na sheria ya tatu ikiwa
ni kuboresha sheria za kodi ikiwa mapato na bima lakini kwa sababu chama
kinaenda kumfia hivyo hataweza kuacha kudandia hoja hata kama hazina
mashiko.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA