Thursday, August 3, 2017
Nafasi za Kazi: Katibu Mahsusi II, Mwendesha Mitambo II, Msaidizi wa Kumbukumbu II
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wananchi wote wenye sifa za
kuajiriwa kuleta maombi yao ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
1.0 KATIBU MAHSUSI III (PERSONAL SECRETARY III)-NAFASI (2) -NGAZI VA MSHAHARA TGS.B
SIFA ZA KUAJIRIWA:
Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha Nne/Sita waliohitimu mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua yaTatu.
Wawe
wamefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno (80) kwa
dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows,
Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
KAZI ZA KUFANYA:
(i) Kuchapa barua na nyaraka za kawaida.
(ii) Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekezniehemu wanapoweza kushughulikiwa. s -
(iii)
Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au
kituellochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
(iv)
Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maafisa walio katika sehemu
alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kurudisha sehemu zinazohusika.
(v)
Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, mladi, wageni, tarehe
za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa
kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumwarifu Mkuu wake kwa
wakati unaohitajika.
2.0 MWENDESHA MITAMBO II (PLANT OPERATOR II)- NAFASA (2) - NGAZI YA MSHAHARA - TGOS A
SIFA ZA KUAJIRIWA:
Mwombaji
awe na Cheti cha Kidato cha nne ambaye ana leseni daraja la G ya
kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo vya aina hiyo, ujuzi sio
chini ya saa 300 (miezi mitatu 3) bila kusababisha ajali
KAZI ZA KUFANYA:
Kuendesha Mitambo chini ya usimamizi wa Dereva wa Mitambo mwenye uzoefu.
3.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II) - NAFASI (1) - NGAZI YA MSHAHARA TGS.B
SIFA ZA KUAJIRIWA:
Waombaji wawe na elimu ya kidato cha Nne/Sita wenye Cheti cha Utunzaji wa kumbukumbu wa fani ya Masjala
KAZI ZA KUFANYA:
(i) Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
(ii) Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
(iii) Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi na somo.
(iv) Kuwekekupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki katika masjala.
(v) Kuweka kumbukumbu; barua, nyaraka nk katika mafaili.
(vi) Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
4.0 MASHARTI YA JUMLA:
(i) Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 usiozidi miaka 45.
(ii)
Waombaji wote waambatishe nakala ya Vyeti vya Taaluma, Vyeti vya Kidato
cha Nne na Sita, Cheti cha Kuzaliwa, picha mbili (2) passport size ya
hivi karibuni iandikwe majina ya mwombaji kwa nyuma.
(iii)
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na mwombaji mwenye
zikiambatishwa na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika na majina ya wadhamini watatu
(referees) wa kuaminika na namba zao za simu.
(iv)
Testimonials na Provisional Results", Statement of Results, hati
matokeo za kidato cha nne (Form IV or VI results slips HAVITAKUBALIWA,
(v) Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA)
(vi) Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
(vii) Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
(viii)Tangazo hili pia linapatikana kwenye Tovuti ya Jiji www.dcc.go.tz
(ix) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Agosti, 2017.
(x) Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika Ofisi za Jiji HAURUHUSIWI, MAOMBI VOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA.
5.0 MAOMBI YATUMWE KWA:
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji,
"Ukumbi wa Jiji"
S.L.P. 9084,
1 Barabara ya Morogoro,
11882 DAR ES SALAAM
6.0
Waombaji waliokidhi sifa wataarifiwa tarehe ya kufanya usaili kwa njia
ya maandishi kupitia magazeti yaliyotumika kutangaza nafasi hizi pamoja
na simu za mikononi au Tovuti: www.dcc.go.tz
Waziri Kombo
KAIMU MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA