Kesi
ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu Tanzania,
Elizabeth Michael (Lulu), imeendelea leo ambapo upande wa mshtakiwa
umeanza kutoa utetezi wake.
Akisimulia
jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, Lulu amesema marehemu alikuwa akimpiga
na panga baada ya kutokea ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi,
alipomuona akiongea na simu.
"Nilikuwa
nataka kutoka ila marehemu 'Kanumba' alinikataza, alikuwa hataki
nitoke, nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na
mimi nilikuwa naogopa kupigwa, mara nyingi alikuwa ananipiga kila
akilewa na sio kwa akili zake, alipoona simu yangu inaita akahisi ni
simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake?
Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku
akinipiga na panga kwenye mapaja", ameelezea Lulu.
Lulu
ameendelea kusimulia...."Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa
nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa, nilimwambia
Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema
anaenda kumuita daktari, alivyosema anaenda kumuita daktari na mimi
nikaondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga, niliondoka
nikawasha gari kuelekea Coco Beach kutuliza akili".
Muigizaji
huyo ameendelea kusimulia kwamba ..."Nilivyofika Coco beach meseji
zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki, nikampigia
'Kidume' ambaye ni rafiki yake Kanumba kumuuliza Kanumba yupo hospitali
gani niende kumuona, akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi,
tukakubaliana tuonane Bamaga, tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka
kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata".
Pamoja
na hayo muigizaji huyo ameithibitishia mahakama kuwa alikuwa na
mahusiano ya kimapenzi na marehemu (Steven Kanumba) kwa muda wa miezi
minne kabla ya kukutwa na mauti.
Mahakama Kuu imeghailisha kesi hiyo mpaka siku ya kesho Oktoba 24, ambapo itasikilizwa tena
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA