Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, amemteua mmoja
wa wajumbe wa Kamati ya Makinikia, Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuchukua nafasi ya Prof. Benno Ndulu
aliyekuwa akiushikilia wadhifa huo.
Rais
Dk. Magufuli ametangaza uteuzi huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam
katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati ya Makinikia
iliyofanikisha kufikiwa makubaliano ya kihistoria baina ya serikali na
kampuni ya Barrick Gold yaliyofungua ukurasa mpya kwa Tanzania kunufaika
zaidi na madini ya dhahabu.
Katika
hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wenyeviti
wa kamati za bunge za madini ya Almasi na Tanzanite, baadhi ya viongozi
wa vyama vya upinzani.
Rais
Dk. Magufuli alimshukuru Spika wa Bunge na Wabunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha hati ya dharura sheria ya madini.
Kwa
upande wake Gavana mteule Profesa Florens Luoga amesema atafanya kazi
kwa uweledi kama sheria za nchi zinavyoelekeza na kuomba ushirikiano kwa
wataalamu wengine wa mambo ya fedha ili kuinua uchumi wa taifa.
Aidha,
Dk. Magufuli alitumia fursa hiyo kuwashangaa watu wanaozusha kuwa
mapato ya nchi yamepungua na kusema kuwa huo ni uongo kwani haiwezekani
serikali ikafanya miradi mikubwa ya ununuzi wa ndege kujenga reli ya
kisasa, kujenga mradi wa umeme wa Stiegler Gorge kama mapato ya nchi
yangekuwa yameshuka.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA