Rais
John Pombe Magufuli amefunguka na kuvitaka vyombo vya dola nchini
viwashungulikiwe watu ambao wamekuwa wakipika data za uongo za serikali
na kuzichapisha sehemu mbalimbali na kusema watu hao wanapaswa
kufikishwa mahakamani.
Rais
Magufuli amesema hayo leo katika hafla ya kuwatunuku vyeti vya pongezi
maaalum kwa wajumbe waliohusika kuchunguza kiwango, aina ya madini
katika mchanga wa madini ambao ni makinikia. Rais Magufuli amesema kuwa
kuna haja Waziri wa Sheria na vyombo vya dola kuangalia namna
inavyowezekana kuwashughulikia watu ambao wanapika data.
"Niwaombe
Watanzania wengi tofauti na wale wachache wanaopiga kelele muwapuuze,
mtu ambaye anabadili data za serikali na kusema kuwa uchumi umeshuka
nadhani wanapaswa kuchukuliwa hatua vyombo vya dola na wewe Profesa
Kabudi ni Waziri wa Sheria muanze kuangalia watu wa namna hii ambao kwao
kubadili Takwimu wanaona kitu kidogo.
"Nafikiri
kuna sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na kunakifungu kinasema mtu
anayebadilisha Takwimu za serikali anaweza kufungwa hata miaka 2 jela,
kwanini hatuvitumii hivi? Unakuta mtu anazungumza makusanyo ya serikali
yameshuka wakati anajua kabisa si kweli" alisema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa mapato ya nchi hayajashuka
ndiyo maana Serikali imeweza kununua ndege zaidi ya sita kwa mpigo,
serikali imeweza kujenga barabara kwa fedha za ndani, na kusema serikali
imeweza kujenga reli kwa kuwa uchumi wake ni mzuri.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA