SETH ASIPTIBIWA HARAKA ANAWEZA KUFARIKI...... PUTO LIMEISHA MUDA WAKE
MSHTAKIWA wa makosa ya uhujumu Uchumi, Harbinder Singh Sethi ambaye ni mmiliki wa IPTL, ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa 'Puto-Balloon' alilowekewa tumbon limeisha muda wake (expire) na asipobadilishwa litamsababishia kifo.
Wakili wa Seth, Alex Balomi mbele ameileza hayo leo Octoba 27 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leornad Swai kueleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kesi iahirishwe.
Katika kesi hiyo Sethi anashtakiwa pamoja na mmiliki mwenza, James Rugemarila ambapo wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Akielezea kuhusu matibabu ya Sethi, wakili Balomi amedai, pamoja na kutekelezwa kwa amri ya mahakama ya kuamuru mshtakiwa akatibiwe Muhimbili, ambapo alipelekwa na kufanyiwa vipimo lakini mpaka leo hajapatiwa majibu ya vipimo wala matibabu.
Amedai kuwa Puto lililowekwa tumboni kwa mshytakiwa limeisha muda wake, na linatakiwa kubadilishwa mwishoni mwa mwezi huu wa Octoba
"Kama hilo balloon halitabadilishwa linaweza kugeuka sumu na kuondoa uhai wake, hivyo daktari aliyechukua vipimo anapaswa kumpatia majibu,". Alidai
Kufuatia hali hiyo ya mteja wake, ameomba upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwani watuhumiwa wanateseka jela bila sababu huku
Akijibu hoja hizo, Wakili Swai amedai mshtakiwa Seth alipelekwa hospital Octoba 13 mwaka huu na kufanyiwa vipimo na daktari, lakini majibu yake ni siri ya Daktari na mshtakiwa na sio vya kuongelea mahakamani.
Alidai kuwa kuhusu upelelezi wanaendelea kufanyia kazi.
Baada ya hayo yote, Hakimu Shaidi amesema mahakama ilitoa amri kwamba Seth apelekwe hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu na amepelekwa, hivyo daktari amekamilisha kazi yake, mawakili wanaweza kwenda kuulizia kuhusu vipimo vyake huko Hospitali
Aidha ameuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika mapema. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10 mwaka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA