Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali
nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za
kulevya.
Uamuzi
huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa
serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya
kutolewa uamuzi.
Katika
uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa
mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo
hicho, ambapo ameona akipokee.
“Mahakama
inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe,
hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo
kinapokelewa,”
Hakimu
Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema
hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake,
hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wakiume.
” Kama upekuzi ungeusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanyika nyumbani kwake,”.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi November 16/2017.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA