Muimbaji
nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na
mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni
takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.
Wawili
hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya
miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao
wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.
Naibu
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza
aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu
la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio
kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda
wa Afrika Mashariki na kati.
Wameanza
kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao
kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo
muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.
“Miaka
14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss,
nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna.
Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa
photoshoot.
Kwa
kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile
za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa
nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.
Kwenye
photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya
na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA