Wakati
kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni na
Siha, zikianza kwa vitimbi, mgombea wa CCM, Maulid Mtulia amewekewa
pingamizi lenye vipengele vitano.
Uchaguzi
huo utakaoshirikisha vyama 12, utafanyika Februari 17 huku ukitarajiwa
kuwa na mpambano mkali baina ya CCM na Chadema inayoungwa mkono na vyama
vitano vya Ukawa ambavyo NLD, NCCR-Mageuzi, CUF ya upande wa Maalim
Seif Sharif Hamad na Chaumma iliyojiunga hivi karibuni.
Uchaguzi
huo unafanyika baada ya waliokuwa wabunge, Godwin Mollel (Siha,
Chadema) na Maulid Mtulia (Kinondoni, CUF) kujivua uanachama kwa maelezo
kuwa wanamuunga mkono Rais John Magufuli na baadaye kujiunga na CCM.
Chama hicho tawala kimewapitisha wawili hao kutetea majimbo hayo bila ya kuendesha mchakato wa ndani.
Kwa
staili kama hiyo, Chadema imemsimamisha Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar),
Salum Mwalimu katika jimbo la Kinondoni na Elvis Mosi (Siha).
Tayari
CCM katika jimbo la Siha na CUF upande wa mwenyekiti anayetambuliwa na
ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba wamezindua
kampeni jana.
Wagombea walirejesha fomu juzi katika ofisi ya jimbo la iliyopo Magomeni.
Lakini
saa chache kabla ya kuanza kampeni, Mwalimu aliwasilisha pingamizi
dhidi ya mgombea wa CCM, akiwa na hoja tano, ikiwemo ya kutofanya
mrejesho wa gharama za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wakili
wake, Frederick Kihwelo amesema kuwa kwanza, Mtulia hajafanya
mrejesho wa gharama za uchaguzi wa mwaka 2015, alipogombea kwa tiketi ya
CUF.
“Jambo
hili hufanywa na mtu yeyote aliyegombea nafasi ya udiwani, ubunge na
urais na haijalishi kama alishinda au kushindwa,” alisema Kihwelo.
“Unapaswa kuandaa mchanganuo wa gharama zako za uchaguzi na kuzipeleka ofisi ya NEC.”
Alisema
hoja ya pili ni Mtulia kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria kwa
kutojaza kwa usahihi fomu zake, kwa madai kuwa zimepigwa muhuri wa
katibu wa CCM badala ya muhuri wa chama hicho tawala.
“Muhuli
ulipigwa katika fomu yake unasomeka wa katibu wa chama badala ya muhuri
wa chama. Hii inaonyesha chama hakijamthibitisha kugombea. Jambo hili
liliwasumbua sana Chadema mwaka 2014 kwa baadhi ya wagombea wao
kuenguliwa, ” alisema Kihwelo.
Alisema
hoja ya mwisho ni Mtulia kujaza fomu akieleza kuwa anajishughulisha na
kilimo cha mbogamboga, jambo ambalo Kihwelo amesema si kweli.
“Hiki kilimo cha mbogamboga amekianza lini kwa sababu tunajua alikuwa mbunge. Tunamtaka athibitishe hili,” alisema.
Msimamizi
msaidizi wa uchaguzi wa Kinondoni, Latifa Almasi alisema wamepokea
mapingamizi lakini haweka wazi idadi yake, na kubainisha kuwa leo
msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Aron Kagurumjuli, atayatolea ufafanuzi
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA