Msanii filamu na video vixen, Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amefunguka na kuomba radhi kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kutokana na vitendo vyake vya kupiga na kuweka picha mitandaoni za nusu uchi.
Akiongea
jana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungiwa na serikali
kujihusisha kufanya kazi zozote za sanaa kwa miezi sita, Pretty Kind
alisema kuwa amejifunza na kugundua kuwa alikuwa anafanya makosa hivyo
sasa hataweza kurudi tena kufanya mambo hayo.
“Naomba
niombe radhi kwa Watanzania wote kwa hiki nilichokifanya natambua
nimefanya kosa naomba msamaha aweze kunisamehe, pia naomba msamaha kwa
mashabiki zangu kwa hiki kilichotokea nimejifunza hivyo nitakuwa Pretty
Kind mwingine mpya na kufanya yale yanayotakiwa katika jamii” alisema
Pretty
Kind amefungiwa kujihusisha na sanaa kwa takribani miezi sita baada ya
kuposti picha katika mtandao wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa nusu
utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Kitanzania na kwenda kinyume
na maagizo ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliyatoa hivi karibuni
kuwataka wasanii wa kike kuvaa kwa staha.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA