Ukuta mrefu unaozunguuka machimbo ya
madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani nchini Tanzania,
umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Ukuta huo wenye urefu wa
kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo
lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na
kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania
pekeeTayari wakuu wa vyombo vya usalama, wametembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za kiTanzania isiyozidi bilioni 6.
Na kusisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA