Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amechukuliwa maelezo katika
Kituo Kituo cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, baada ya kukamatwa jana
kwa tuhuma za kufanya mikutano kinyume na sheria.
Wakili
wa Zitto Emmanuel Lazarus Mvula, amesema Polisi inatuhumu ziara ya ACT
ya kutembelea madiwani wa chama hicho katika kata mbalimbali kwenye
mikoa nane kwamba ni kosa kisheria.
“Ndugu
Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya sheria ya
kanuni ya adhabu, lakini kosa hilo amefunguliwa peke yake tu. Baada ya
kuandika maelezo tokea saa 4:42 usiku wa jana mpaka 5:40 usiku, Jeshi la
Polisi wamekataa kumpa dhamana kwa maelezo wanasubiri maelekezo kutoka
juu,” amesema.
Wakili Mvula ameeleza kuwa, Zitto amewekwa mahabusu katika kituo kikuu cha polisi Morogoro.
“Polisi
imekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti
yake ni yapi, na wamekataa kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa
mujibu wa sheria au la,” amesema.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA