Msanii
wa muziki Bongo na Video Vixen, Gigy Money amejibu iwapo amerudiana na
mpenzi wake Mo J baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja na mtoto wao.
Mwanadada huyo maarufu mtandaoni akizungumza na Wasafi TV amesema ni kweli kwa sasa wapo pamoja na hawajawahi kuachana.
"Unajua
kuachana ni maneno tu tunakuwa tunaongea, halafu tukiachana sisi kwa
ajili tayari ni wazazi kimaadili yetu tutakuja kukutanishwa tu na yule
mtoto pale ndani, angalieni tu vitendo (tumerudiana)," amesema Gigy
Money.
Utakumbuka
baada ya Gigy Money kujifungua kuliibuka mvutano kati yake na Mo J
ambaye ni Mtangazaji wa Choice FM kwa madai kuwa mtoto si wake baadaye
zikaibuka tuhuma nyingine kuwa hatoi matunzo kwa mtoto lakini sasa
wameonekana pamoja na wenye furaha.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA