Mkazi
wa Kijiji cha Luhega, Wilaya ya Tanganyika, Milembe Manoni (22),
amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani, kisha mwili wake
kufungiwa ndani banda ng’ombe.
Akizungumzia tukio hilo jana, kaka wa marehemu, Nestory Malongo alisema lilitokea juzi usiku nyumbani kwa marehemu.
Alisema taarifa ya kuuawa kwa Milembe aliipata saa tatu asubuhi na wasamalia wema,
Baada ya kapata taarifa hizo, alikwenda eneo la tukoo na kukuta watu wengi wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba.
Alisema baada ya kuona mwili hiyo, waliona majereha sehemu za kifuani ambayo inaonyesha alichowa na kisu.
Alisema
polisi walifika eneo hilo, kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili
ya kwenda kuufanyia uchunguzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi .
Mama wa marehemu, Tuma Matine alisema alipigiwa simu na mkwe wake na kusisitiza kitendo hicho ni cha kikatili mno.
Alisema
katika nyumba hiyo, binti yake alikuwa kuwa akiishi na mfanyakazi
mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mifugo ya ng’ombe.
“Nasikitika baada ya tukio hili huyu mfanyakazi hajaonekana nyumbani…inawezekana wazi ndiye aliyehusika na kifo hiki,”alisema.
Mwenyekiti
wa chama cha wafugaji wa mifugo wa Mkoa wa Katavi, Mussa Kabushi
alisema kumekuwapo na mauaji ya mara kwa mara ya kuuawa kwa wafugaji.
Alisema
mauaji hayo, yamekuwa yakisababishwa kutokana na tabia ya wafugaji
kukaa kwenye maeneo ya kujitenga na kutokuwa na ulinzi.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa
mauaji hayo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Credit: mtanzania
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA