- Liverpool ndio mabingwa wa kombe la ligi ya mabingwa Ulaya kwa mara ya sita baada ya kuilaza Tottenham katika mechi ilioshirikisha timu mbili za Uingereza mjini Madrid.
Baada ya penalti hiyo, kipindi kilichosalia cha mchezo hakikuwavutia wengi kutoka timu zote mbili hadi pale Divock Origi aliyefunga magoli mawili katika nusu-fainali dhidi ya Barcelona alipoifungia Liverpool goli lao la pili.
Ni kombe la kwanza la Liverpool chini ya ukufunzi wa Klopp, ambaye alikuwa amepoteza fainali sita ikiwemo fainali mbili za kombe la mabingwa Ulaya.
Na Tottenham waliposhindwa kusawazisha waliadhibiwa na Divock Origi aliyingia kama mchezaji wa ziada na kuhakikisha kuwa mkufunzi Jurgen Klopp anashinda kombe lake la kwanza kama Mkufunzi wa Liverpool baada ya kupiga mkwaju wa kimo cha nyoka uliomuwacha bila jibu kipa wa Spurs Hugo Lloris huku ikiwa zimesalia dakika tatu.
Mkufunzi wa Spurs Mauricio Pochettino alifanya uamuzi wa bahati nasibu bada ya kumchagua nahodha wa klabu hiyo na Uingereza Harry Kane kushiriki katika mechi hiyo licha ya yeye kutoshiriki katika mechi tangu mwezi Aprili kutokana na jeraha la kifundo cha mguu, akichukua mahala pake Lucas Moura aliyefunga magoli matatu dhidi ya Ajax.
Liverpool walishinda kombe hilo ambalo liliwaponyoka msimu uliopita nchini Ukraine na sasa wako nyuma ya Real Madrid na AC Milan kama klabu zilizoshinda kombe hilo kwa mara nyingi.
Kipenga cha mwisho kilizua sherehe kubwa miongoni mwa wachezaji , wasimamizi wa timu pamoja na mashabiki waliojaa katka uwanja wa Wanda Metropolitan.
Kitu kimoja ambacho hakitasahaulika wakati Liverpool iliposhindwa na Real Madrid katika fainali ya kombe hilo msimu uliopita ni picha ya Mo salah akionekana kububujikwa na machozi baada ya kupata jeraha la bega wakati walipokuwa wakipigania mpira na Sergio Ramos.
Ulikuwa wakati ambao ulibadilisha hamu ya mchezo huo ndani ya uwanja huo huku Liverpool ikishindwa kubadili matokeo.
Klopp afuta msururu wa bahati mbaya
Mkufunzi wa Liverpol Jurgen Klopp alijua kwamba mkosi mkubwa wa fainali ya kombe la mabingwa ni kupoteza mara sita fainali ya kombe hilo.
Alikuwa amepoteza mara ya tatu na Liverpool ikiwemo katika kombe hilo msimu uliopita na huku ikiwa hakuna mtu ambaye anaweza kushuku kazi nzuri ya raia huyo wa Ujerumani ni mtangulizi wake katika uawaja wa Anfield Bill Shankly aliyesema kuwa wa kwanza ni wa kwanza na wa pili hajulikani.
Sasa Klopp amejivua gwanda hilo la bahati mbaya na badala yake kujulikana kama mkufunzi ambaye aliipandisha Liverpool katika kilele cha michuano ya Ulaya
Hatahivyo kiwango cha mchezo hakitamjalisha mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye alipoteza fainali ya kombe hilo mwaka uliopita kwa Real Madrid.
Hatua ya Tottenham kumuanzisha mshambuliaji Harry Kane ambaye alikuwa akiuguza jeraha kwa kipindi cha miezi miwili haikuzaa matunda.
About Mr PinkMoja@ TZ
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA