Iran imezindua mfumo wa kujilinda kwa makombora unaoweza kulenga shabaha sita za adui kwa wakati mmoja.
Mfumo
huo wa makombora uliopewa jina la Khordad 15 umezinduliwa mbele ya
Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Brigedia Jenerali Hatami amesema kuwa, mfumo wa
makombora wa Khordad 15 una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni
kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita
120.
Ameongeza
kuwa mfumo huo wa makombora aidha una uwezo wa kugundua maeneo ya siri
na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45.
Waziri
wa Ulinzi wa Iran ameeleza pia kwamba mfumo wa ulinzi wa Khordad 15
unatumia makombora ya Sayyad 3; na una uwezo wa kugundua, kusambaratisha
na kutungua shabaha sita kwa wakati mmoja.
Iran imeeleza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujilinda na si tishio kwa nchi nyingine.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA