Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Juni 11, 2019 imetoka hati ya
kumkamata mwigizaji , Wema Sepetu baada ya kukiuka masharti ya dhamana.
Uamuzi
huo umetolewa na Hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira
Kasonde baada ya mshtakiwa kushindwa kufika mahakama kusikiliza kesi
inayomkabili.
Kabla
ya kutoa uamuzi huo wakili wa Serikali, Silyia Mitanto amedia kesi
hiyo ilikuja kwa ajili ya kusikiliza ushahidi lakini Wema na mdhamini
wake wote hawakuwepo mahakamani.
Baada
ya kueleza hayo, Ruben Simwanza ambaye ni wakili wa Wema amesema mteja
wake alikuwepo katika mahakama hiyo lakini aliugua tumbo na kulazimika
kuondoka.
Baada
ya kusikiliza maelezo ya pande zote, hakimu Kasonde amesema, “Kama
amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama
itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani.”
Baada ya kueleza hayo hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4, 2019 huku akitoa hati hiyo ya Wema kukamatwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA