Dar es Salaam. Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameahirisha kesi hiyo mpaka kesho Jumanne Novemba 2, 2021.
Hiyo ni baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na shahidi wa nne kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo yaliyofanyika leo Jumatatu Novemba 2, 2021.
Jaji Joachim Tiganga ameingia mahakamani na kesi inaitwa na washtakiwa wanapanda kizimbani.
Mawakili wa Serikali wanajitambulisha wakiongozwa na Wakili wa Serikalia Mwandamizi, Robert Kidando
Jopo la mawakili wa utetezi nalo linatambulishwa na kiongozi wa jopo, Peter Kibatala.
Jaji anawaita washtakiwa kwa namba zao katika kesi mmoja mmoja nao wanasimama kuoneaha kwamba wote wapo mahakamani.
Jaji anawaita washtakiwa namba moja namba mbili namba tatu na namba nne.
Wakili wa Serikali leo tuna shahidi mmoja na tuko tayari kuendelea.
Shahidi wa nne anaingia mahakamani na anapanda kizimbani.
Jaji anauliza atakuwa shahidi wa nne?
Upande wa mashtaka wanajibu ndio.
Anajitambulisha Anisha Valerian Mtalo (45), Mchaga, Mkristo RC na mfanyabiashara
Anaapa kiapo cha ukweli.
Anaongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Martin
Naishi Moshi Rao Madukani
Nafanyabiashara ya kuuza mbege kwa miaka minane sasa.
Eneo la biashara yangu mbele Kuna fremu za maduka, grocery, steshenari na sehemu ya kutolea movies.
Agosti 5, 2020 nilikuwa sehemu yangu ya biashara majira ya saa 7 kasoro mchana, nilifanya usafini
Kabla nilikuwa nimetokea nyumbani kwenda saluni kuosha nywele
Nilipotoka saluni niliipitia kumsalimia ndugu yangu nikakata wakaka wamekaa wanakunywa bia
Pia walikuwa wanasajili laini. Kuna kijana huwa anapita mitaani kusajili laini.
Niliendelea na usafi, kuna wakaka wawilibwalukuwa wnapitapita wakiongea na simj wanaenda wanarudi wakiongea na simu.
Ni wale waliokuwa wanakunywa pombe
Kutoka kwenye eneo la biashara yangu mpaka kwenye grocery ni kama hatua 10 na hapo katikati pana uwazi.
Baada ya muda hao wakaka waliokuwa wanaongea na simu, wakstokea watu wawili wakasema jwa sautii kubwa mko chini ya ulinzi mnahusika na mambo ya ugaidi, chuchumaa chini, wakachuchumaa. Hao walikuwa Ni maaskari.
Wakati huo nilikuwa barazani, kutoka hapo mpaka hapo kwa hao askari kuna kama hatua tano.
Walitii sheri wakakaa chini wakanyoosha mikono juu
Walikuwa ni askari wawili
Baada ya hapo haoi ya pale ilikuwa ni tulivu.
Baada ya hapo walikuja maaskari wengine watatu eneo la tukio.
Baada ya kufika wakawa watano, akatoa mmoja akasema anaomba nisogee karibu anahitaji kuwafanya upekuzi. Huyo akijitambulisha kuwa anaitwa Askari Polisi Jumanne.
Nikajiridhisha kwa sababu alitoa kitambulisho akanionesha.
Baada ya hapo Askari Jumanne alijipekua kuanzia kichwani mpaka miguuni akasema mnaona sina kitu chochote. Mimi nilikuwa na dada mmoja anaitwa Sophia.
Kutoka pale walipokaa chini wale vijana na mimi niliyokuwa ilikuwa kama hatua mbili. Kuna baadhi ya watu raia walikuja baada ya kusikia ile sauti kaa chini mko chini ya ulinzi. Hali ilikuwa imetulia.
Jumanne alimsimamisha mmoja akamuulizanunaitwa nani akajibu anaitwa Adamu Hassan Kasekwa.
Akiwa amenyoosha mikono juu alimwambia geuka akageuka.
Baada ya kugeuka Askari Jumanne alianza kumpekua kuanzia kichwani, mabegani kifuani akipofika kiunoni akakuta kitu upande wa kushoto kiunoni. Nilikiona ilikuwa ni bastola.
Afande Jumanne akitwambia kuwa ni bastola na baada ya hapo alituonesha namba A5340
Alituonesha kutoka kwenye hiyo bastola.
Wakati huo Adamu alikuwa amesimama. Niliona hizo namba na risasi tatu.
Baada ya hapo akaendelea na upekuzi mfuko wa kulia alikuta vikete vidogovidogo vimefungwa akatwambia inasadikuwa ni dawa za kulevya lakini itajulikana mbele ya safari. Vilikuwa 58 vimefungwa kwenye nailoni.
Aliendelea kumpekua akakuta simu aina ya Itel akaifungua akato la laini akampa yule Askari wa pembeni.
Kisha akamwambia askari wa pembeni naomba fomu akatoa fomu mbili.
Kwenye ile fomu aliandika vitu alivyokuwa amempekua
Fomu ya kwanza alikuwa amejaza bastola. Risasi simu na laini nakumbuka kulikuwa na laini ya Voda na Airtel.
Alimpa akasoma akasaini, halafu akasaini yeye na baadaye akaomba tusome.
Yaani alimpa Adamu akasaini.
Aliletewa fomu nyingine, alijaza vile vikete vidogovidogo, 58. Alimpa Adamu akasoma akasoma akasaini, Kisha akasaini yeye Askari akatupa mimi na dada Ester tusaini
Alimwambia yule mwingine asimame na huyu wa kwanza alichuchumaa. Aliuliza jina (wa pili) aksema anaitwa Mohamed Abdillahi
Alimwambia asimame ageuke, baada ya kugeuka akaanza kumpekua.
Alianzia kichwani mabegani kifuani kiunoni. Upande wa kulia alimkuta na vikete vidogovidogo navyo vimefungwa mfuko wa nailoni, vilikuwa 25.
Alimpa Askari wa pembeni akaendelea kumpekua akamkuta na simu aina ya Tecno. Nayo akaifungua akatoa laini, akaandika namba. Nakumbuka kulikuwa kuna Halotel na Airtel. Alimpa yule Askari wa pembeni zile laini.
Akaendelea na upekuzi lakini hakukuta kitu kingine
Baada ya kumaliza alimuomba askari ampe fomu, alimpa fomu mbili. Fomu ya kwanza alijaza vile vikete vidogovidogo, vilikuwa 25. Alimpa Mohamed akasoma halafu akasaini baadaye akasaini afande Jumanne halafu akatupa Mimi na dada Ester tusaini.
Baada ya hapo Ile fomu nyingine alijaza simu na zike laini mbili za Halotel na Airtel.
Alimpa Mohamed akasoma akasaini, Afande Jumanne naye alisaini na akatuomba na sisi tusaini Mimi na dada Ester
Baada ya kumaliza upekuzi walivalishwa pingu. Afande Jumanne akasema twende nao kituoni tukatoe maelezo. Waliovakishwa pingu nia Adamu na Mohamed
Baada ya kuvalishwa pingu walielekea kwenye gari.
Eneo la tukio kulikuwa na askari watano. Kuna wawili walikuwa wamebeba bunduki. Hali ya hewa siku hiyo kulikuwa na jua na mwanga wa kutosha. Ilichukua kama dakika 45 pale eneo la tukio.
Tulienda Central Moshi. Baada ya kufika pale tulitoa maelezo, tuliandika maelezo yetu kuhusiana na tukio hilo.
Hizo fomu zilizojazwa nikiziona hapa naweza kuzitambua kutokana na vitu vilivyoandikwa na kuna jina langu. Vitu hivyo ni bastola nyeusi na namba A5340 na risasi.
Wakili anampa shahidi nyaraka anamtaka aingalie na kisha aseme ni nini.
Shahidi anasema ndio yenyewe fomu aliyosaini na ameitambua kutokana na vitu vilivyopo na jina lake Anitha Vakerian Mtalo.
Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunaona shahidi anakwenda kwenye details za nyaraka na hivyo tunaomba jibu hilo liondolewe kwenye rekodi.
Wakili Martin: Shahidi unaomba mahakama hiyo ifanye nini kuhusu fomu hiyo,
Shahidi: Naiomba mahakama iipokee kama kielelezo cha ushahidi wangu.
Mawakili wa utetezi baada ya kuikagua fomu hiyo mmoja baada ya mwingine waksema kuwa hawana pingamizi.
Jaji Tiganga: Basi Mahakama inaipokea kwa utambuzi kama ID1
Wakili wa Serikali anaendelea kumwongoza sahidi. Shahidi anaeleza kuwa hiyo bastola anaitambua kwa rangi yake nyeusi na risasa zilikuwa ni za dhahabu.
Wakili Martin anaomba bastola hiyo ambayo ilishapokewa kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka anampa shahidi anaiangalia na anamuiliza ni nini na
Shahiidi anajibu ni bastola ambayo aliiona kutoka kwa Adamu na kwamba ameigundua ni yenyewe kwa nambazake A5340 ambazo anazionyesha.
Wakili: Hao watu Adamu Hassani Kasekwa na Mohamed, hao watu ukiwaona unaweza kuwatambua?
Shahidi: Ndio naweza kuwatambua
Wakili: Wako hapa mahakamani?
Shahidi: Ndio.
Wakili: Wako wapi?
Sahidi: Pale mbele.
Shahidi anawatambua wasahtakiwa akianisha mavazi akianza na Mohamed kuwa amevaa t-shirt ya mistari ya kijani na myeupe na Adamu amevaa shati lenye rangi nyeupenyeupe.
Wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya anaanza kumuuliza shahidi
Wakili Mtobesya: Naomba unionyeshe uliposaini
Unasema ulisaini nyaraka ngapi?
Shahidi: nilisaini nyaraka nne
Wakili: Mheshimiwa Jaji kulingana na sheria ya ushahidi tunaomba shahidi asaini sehemu nyingine ili tuweze kulinganisha.
Wakili Mtobesya: Mheshimiwa naomba mahakama iweze kuruhusu witness asaini saini nyingine ili mahamama iweze ku-compare signature zake maana kuna nyaraka nyingine nataka kuitumia lakini wenzetu wa upande wa mashtaka wanaweza wakasimama. Naomba chini ya kifungu cha 75 cha Sheria ya Ushahidi
Jaji: Hicho kifungu kinaielekeza mahakama kumruhusu kusaini hapa?
Wakili Mtobesya: Sababu kuna document nataka kuitumia lakini wenzetu wanaweza kusimama.
Jaji: Kwa hiyo tutakuwa tumeitengeneza hapa mahakamani. Unachotaka kufanya ni kuingilia mahakama katika kutengeneza ushahidi hapa. Kwa hiyi wewe jaribu tu kutumia hiyo document tuone kama upande wa mashtaka wanaweza kusimama.
Wakili Mtobesya: Basi sawa Mheshimiwa.
Wakili Dickson Matata anasimama na kutoa ufafanuzi kuwa chini ya kifungu cha 75(2) cha Sheria ya Ushahidi mahakama kumwelekeza shahidi kusaini nyaraka ili kujiridhisha.
Hoja ya wakili Matata inaungwa mkono na Wakili John Mallya
Wakili wa Serikali Kidando: Hayo maombi yaliyowasilishwa na Wakili Mtobesya ni mapema sana ingawa Mahakama ina mamlaka hiyo kama kungekuwa na nyaraka nyingine yenye utofauti.
Hapa hapa mahakamani hatutafuti ushahidi labda endapo kungekuwa na nyaraka nyingine ambayo inautofauti.
Jaji Tiganga: Mimi tafsiri yangu mahakama imepewa mamlaka ya kufanya ulinganisho wa maneno au namba ikimaanisha mtu ambaye mahakama inaweza kumwelekeza anayo maarifa kuliko mahakama, ni mtu mjuzi kuliko mahakama yenyewe.
Jaji Tiganga: Kwa hiyo mimi nadhani ungeitumia nyaraka hiyo ili mahakama ifanye ulinganisho huo kama upande wa mashtaka watapinga sasa ndio mahakama itashughulikiakupiga huko.
Jaji: Sawa na mimi nakubali mahakama inayo mamlaka hayo ya kufanya ulinganisho huo lakini siyo nyaraka aliyosaini mahakamani maana hatujui itakuwa ni ya namna gani.
Kwa hiyo wewe endelea kutumia hiyo uliyo nayo kama watapinga upande wa mashtaka tutashughulikia kupinga huko.
Licha ya Jaji kumruhusu wakili Mtobesya kutumia nyaraka aliyonayo anaomba nyaraka ambayo ni halisi, ambayo haijachapwa akisema kuwa kwa kuwa nyaraka hizo ziliwekwa wazi wakati wa washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi, na kwamba kwa kuwa washtakiwa walipewa ili kuwawezesha kujua aina ya ushahidi unaoletwa mbele yao na wajue namna ya kujitetea hivyo na wao mawakili wana haki ya kuzitumia.
Na kwamba kwa kuwa washtakiwa walipewa ili kuwawezesha kujua aina ya ushahidi unaoletwa mbele yao na wajue namna ya kujitetea hivyo na wao mawakili wana haki ya kuzitumia.
Hata hivyo Wakili wa Serikali Kidando anapinga akisisitiza kuwa hicho ni kielelezo chao wanachokusudia na hivyo wao utetezi hawana haki ya kuzitumia kwa utaratibu ambao Mtobesya anautaka.
Badala yake anasema atumie utaratibu wa kuwasilisha maombi maalumu chini ya kifungu cha 68 cha Sheria ya Ushahidi.
Baada ya kurejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani kuhusiana na suala kama hilo anahitimisha kwa kuiomba mahakama iyatupilie mbali maombi hayo akininisha kuwa kama mahakama itakubali utaratibu huo basi mahakama itakuwa imeingizwa katika hatua isiyo sahihi.
Wakili Mtobesya anasisitiza kuwa wanayo haki hiyo kwa kuwa shahidi huyo ni wao upande wa mashtaka na wao utetezi hawana muda mwingine wa kuwa naye tena huyo shahidi baada ya sasa, hoja ambayo inaungwa mkono kwa msisitizo na wakili Nashon Nkungu.
Jaji: Hoja zako (Mtobesya) unezijenga katika mazingira matatu kwanza kwamba ni haki ya mshtakiwa anapopelekwa Mahakama Kuu na nyaraka hizo huwa anapewa ili kumwezesha mshtakiwa kujitetea.
Jaji: Jambo la pili umesema kwa kuwa ni ushahidi wa upande wa mashtaka na wanakusudia kuutumia.
Jaji: Na tumesikia namna upande wa mashtaka walichojibu yapo ilikuwa off record basi sasa niwape nafasi sasa ya kukusikilizeni ili mahakama itoe uamuzi, au mnaonaje?
Mtobesya: Mheshimiwa nadhani tusiipe mahakama kazi ya kuandika nadhani tuafikiane tu.
Jaji: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Wakili Kudando: Ni sawa Mheshimiwa Jaji.
Jaji: Basi tupate ahirisho dogo na tutarudi hapa baada ya dakika kumi. Jaji Tiganga anaahirisha kesi.
Mahakama imerejea baada ya ahirisho fupi
Wakili wa utetezi Mtobesya anaendelea kumuhoji shahid
Wakili Mtobesya: unakumbuka nani aliandika maelezo yako
Shahidi: Afande Jmanne
Wakili: Ulipoyaandika uliyasoma na kuona yako sahihi
Shahidi: Ndio
Wakili: Shahidi unajua kusoma na kuandika
Shahidi: Ndio
Wakili: Shika hizo karatasi angalia kama kuna majina yako na askari aliyeandika.
Wakili: Hebu isome kuanzia hapo juu kwa sauti kila mtu asikie
Wakili: Soma hatu kwa hatua Mahakama inataka kujua
Baada ya shahidi kumaliza kusoma maelezo aliyoyaandika polisi.
Wakili Mtobesya: Nitakurudisha kwenye maeneo baadhi uliyosoma
Itakuwa sahihi uliiambai Mahakama wale askari walipofika aliwatajia majina
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwenye hayo maelezo kuna sehemu pameandikwa chini ya ulinzi
Shahidi: Hayapo
Wakili: Ni sahihi wakati unashuhudia wakikamatwa ulikuwa unafanya usafi
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwenye hayo maelezo kuna sehemu yameandikwa
Shahidi. Hapana
Wakili: Kwenye hayo maelezo kuna sehemu imeeleza hao askari walitoa kitambulisho kabla ya upekuzi.
Shahidi: Hapana
Wakili: Washtakiwa kabla ya kufanyiwa upekuzi kuna sehemu inasema walijitambulisha kwenye hayo maelezo kuna sehemu imeandikwa
Shahidi: Hapana
Wakili Mtobesya: Iambie Mahakama jina la Adamu ulilifahamu kabla ya upekuzi au baada
Shahidi: Baada ya kupekuliwa
Wakili: Itakuwa sahihi uliieleza Mahakama ulisaini nyaraka nne
Shahidi: Ndio
Wakili: Ntakuwa sahihi nikisema ilisainiwa nyaraka moja na sio nne kama ulivyosema
Shahidi: Kwa mujibu wa mustari huu ni kweli
Wakili: Nisomee hapo kwenye hiyo nyaraka
Wakili: Nitakuwa ni sahihi uliieleza Mahakama aliyesaini ni Jumanne
Shahidi: Sikusema alikuwa ni afande ambaye sikumfahamu
Wakili: Ungependa maelezo yawe sehemu ya ushahidi siku ya leo
Shahidi: Ndio ningependa
Wakili Mtobesya: Ndio hayo tu Mheshimiwa
Jaji: Mahakama inayapokea maelezo hayo kama sehemu ya ushahidi.
Wakili Mtobesya: Naomba kuendelea.
Kwenye maelezo yako umesema ulisaini hati zaidi nne.
Shahidi:Ndio
Wakili: Mueleze Mheshimiwa zilijazwa na nani
Shahidi: Afande Jumanne
Wakili: Na wewe ulisaini nyaraka zote
Shahidi: Ndio
Waki: Ulisaini upande gani
Shahidi: Pembeni
Wakili: Ieleze Mahakama zilikuwa zinamuhusu mtuhumiwa gani
Shahidi: Nilizosaini upande wa kulia zilikuwa zinamuhusu Adamu
Wakili: Na zilizokuwa zinamuhusu Mohamed
Shahidi: Nilisaini kushoto
Wakili: Zote ulisaini mwenyewe na kwa mkono wako
Shahidi: Ndio
Wakili: Na sahihi zote zinafanana ukiwa chini ya kiapo
Shahidi: Sio zote kutokana na hali
Wakili: Mweleze Jaji ulikuwa kwenye hali gani
Shahidi: Nyingine nilisaini nikiwa nimesimama na nyingine kituoni nikiwa nimekaa
Wakili Mtobesya: Hiyo ndio hali inayosababisha sahihi zisifanane
Shahidi: Ndio
Wakili: Ulisesma hati ulisaini sehemu ya tukio
Shahidi: Kuna nilizosaini wakati nimekaa na nyingine wakati nimesimama
Wakili: Zipi amabazo zinatofautiana
Shahidi: Niliyokuwa nimekaa
Wakili: Zote ulizosaini ukiwa umesimama zinafanana
Shahidi: Zinafanana
Wakili: Mheshimiwa Jaji naomba kuishia hapo
Wakili wa utetezi Mallya anaanza kumuuliza maswali shahidi
Wakili Mallya: Bado unafanya biasshara ya mbege
Shahidi: Ndio
Wakili Mallya: Inalewesha au hailewesjhi
Shahidi: Ipo inalewesha na nyingine haileweshi
Wakili: Una ndugu ambaye ni polisi
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulijuaje kitambulisho ni cha polisi
Shahidi: NIlion chapa ya Taifa
Wakili: Na kingine
Shahidi: Jina
Wakili: Lilikuwa limeandikwaje
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Unasema umbali ulipokuwa na Watuhumiwa ni umbali gani
Shahidi: Hataua kumi
Wakili: Umbali wa hatua kumi unaona vizuri
Shahidi: Ndio naona vizuri
Wakili: Kuna mtuhumiwa umesema amevaa tisheti ya mistari Myeusi, unataka Mahakama ikuamini unaona vizuri.
Shahidi: Kimya
Jaji: Tupe jibu basi
Shahidi: Macho yangu yana shida sema leo nimesahau kuvaa miwani
Wakili: Umeieleza Mahakama kama siku hiyo ulivaa miwani
Shahidi: Hapana
Wakili: Uliiomba mahakama upewe miwani
Shahidi: Sikuomba
Wakili: Unajua usajili unatumia vitambulisho
Shahidi: Ndio
Wakili: Na wewe uliona wakisajili
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwenye maelezo yako kuna sehemu uliandika vitambulisho vyao
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulisema walikuwa wana kunywa bia
Shahidi: Ndio
Wakili: Kuna sehemu uliandika fedha mlizowakuta nazo kuna sehemu zimeandikwa
Jaji: Walikuwa wameshalipa
Mahakama kicheko
Wakili Mallya: Zoezi la usafi lilichukua muda gani
Shahidi: Kama dakika kumi
Wakili: Kitendo cha polisi kuwakamata na kukuita wewe ilichukua muda gani
Shahidi: Kama dakika 3
Wakili: Zoezi la upekuzi lilichukau muda gani
Shahidi: Kama dakika 45
Wakili wa Mallya: Tuamini maneno yako au maelezo yaliyoandikwa
Shahidi: Tuchukue yote
Wakili Mallya: Umeulizwa na wakili Mtobesya aliyekuchukua maelezo kituoni ni nani
Shahidi: Sikumbuki
Waki: Alikuwa Jinsia gani
Shahidi: Wakiume
Wakili Mallya: Sahihi hii na hii zinafanana
Shahidi: Hazifanan lakini ni zangu
Wakili Mallya: Kiongozi wa hao askari alikuwa anaitwa nani
ShahidI: Jumanne
Wakili: Unamfahamu Kingai
Shahidi: Hapana
Wakili: Unasema walikuwa askari kujitambulisha
Shahidi: Alikuja mmoja
Wakili: Watuhumiwa walikuwa wangapi
Shahidi: Wawili
Wakili Mallya: Ndio hayo tu Mheshimiwa
Mahakama imerejea baada ya mapumziko ya muda mfupi
Wakili wa utetezi Dickson Matata anaanza kumuuliza shahidi maswali
Wakili: Ulisema unaishi hapo hapo Rau madukani
Shahidi: Ndio
Wakili: Ni kata au
Shahidi: Ndio
Wakili: Wakati unahojiwa ulisema ni kata
Shahidi: Hapana
Wakili: Ni kweli hujatutajia mtaa unatoka
Shahidi: Sijaulizwa
Wakili: Hujasema kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au kwako
Shahidi: Nimepangisha
Wakili: Ni sahihi hujatuletea mkateaba wa nyumba
Shahidi: Sijaulizwa
Wakili: Hujatutajia hata mwenye nyumba
Shahidi: Sijaulizwa
Wakili: Umetuambi unafanya biashara ya mbege
Shahidi: Ndio
Wakili: Hujatuambia kama hiyo mbege unatengeneza au una nunua
Shahidi: Sijaulizwa
Wakili: Hapo unapofanya biashara uhujaseamakama ni kwako au umepangisha
Shahidi: Nimepngisha
Wakili: Miaka nane unafanya kazi hapo hujatutajia hata jina la saaluni
Sahidi: Sijaulizwa
Wakili: Hujatuletea mkataba
Shahidi: Sikuwambiwa nije nao
Wakili: Ulisema uliona vijana wawili wanaokunywa bia
Shahidi: Niliona watatu
Wakili: Ni sahihi ulisema walikuwa wanasajili laini
Shahidi: Walikuwa wanasajili laini
Shahidi: Walikuwa wamekaa na kijana anayesajili
Wakili: Mahakama ichukue lipi
Shahidi: Yote
Wakili: Mtu anaweza kuwa anafanya yote kwa wakati mmoja
Sahid: Ndio
Wakili: Ulisema mlienda central polisi
Shahid: Ndio
Wakili: Ulisema ni muda gani mlitoaka pale
Shahidi: Sijaulizwa.
Wakili: Kwenye maelezo yako wapi Ester ametajwa
Shahidi: Hajaandikwa
Wakili: Ni hayo Mheshimiwa
Wakili wa utetezi Peter Kibatala anaanza kumhoji shahidi
Wakili: Sasa hivi ni sangapi?
Shahidi: Saa tisa kasoro
Wakili: Umeona wapi
Shahidi: Kwenye saa
Wakili: Unaoana pale nje
Shahidi: Ndio
Wakili: Yale magari yana rangi gani
Shahidi: buluu na nyeusi
Wakili: Wakati unakuja hapa umetoka wapi
Shahidi: Gesti
Wakili: Mara ya mwisho kuwa Rau ni lini
Shahidi: Ijumaa
Wakili: Aliyekuuzia mbege mwezi wa tano mwaka huu ni nani
Shahidi: Mama Kazi Moto, Paulo
Wakili: Majina yako mengine ni mama Pendo
Shahidi: Mama Pendo na mama Peter
Wakili: Ni kweli huwa husimama mwenyewe
Shahidi: Nasimama mwenyewe
Wakili. Ni muda gani binti yako huwa anakuwa pale
Shahidi. Alianza Jumamosi
Shahidi. Huwa anisaidie tu usafi
Wakili: Mwambie Jaji katika ushahidi wako ulimtaja Pendo
Shahidi: Sikuzungumza
Wakili Kibata: Pale Rau kuna mtu ana duka jumla na vipodozi na fremu nne
Shahidi: Ndio
Wakili: Na upande mwingine wanaunza vinywaji
Shahidi: Ndio
Wakili: Anaeuza hapo huwa anakaa mbele ya duka lake
Shahidi: Ndio
Wakili. Hii picha unayoionyesha hapa ndio ulimweleza Jaji
Shahidi: Hapana
Wakili: Wakati bastola inatolewa uliona
Shahidi: Ndio
Wakili: Ulimsachi wewe
Shahidi: Hapana
Wakli: Ulijuaje ni kitu kigumu
Shahidi: Baada ya kutolewa
Wakili: Ulisema zilipatikana Risasi tatu kwenye magazine
Shahidi: Ndio
Wakili: Meonyeshwa hapa mahakamani
Shahidi: Hapana
Wakili: Risasi tatu zilikuwa kwenye magazine unafahamu magazine inapokaa
Shahidi: Iko kwa chini
Wakili: Ulifanya zoezi la kumuonyesha Jaji
Shahidi: Sikumuonyesha
Wakili: Katika maelezo yako hakuna mahali uliposema kuna polisi alichomoa Magazine ili muone mahali risasi zilipo
Shahid: Nimesema
Wakili: Kuna sehemu yoyote uliemwambia Jaji huyu mwandishi kuna kitu amekiacha
Shahidi: Hapana
Wakili: Hakuna mahali popote kuna askari ametajwa zaidi ya Jumanne
Shahidi: Sikumtaja
Wakili: Ni kwakuwa hawakujitambulisha au umesahau
Shahidi: Ni muda mrefu
Wakili Kibata: Umefafanua wale watu wengine wawili ni kina nani
Shahid: Hapana
Wakili: Uliambiwa hayo maezo ni ya kisheria au mapambo
Shahidi: Niliambiwa ni ya onyo
Wakili: Hakuna mahali umetaja jina Adamoo
Shahid: Hakuna
Wakili: Mjini katika hati ya utambuzi kuna mahali pameandikwa Adamoo
Shahidi: Hakuna
Wakili: Unajua majibu ya ushadi wako yakitofautiana yananathiri mwenendo wa kesi
Shahidi: Ndio
Wakili: Jina Adamoo lipo au halipo
Shahidi: Lipo
Wakili: Wewe ni muongo sio muongo
Wakili wa Serikali Kidando anasimama Mheshimiwa Jaji suala la yeye ni mkweli au sio mkweli aiachie Mahakama
Wakili: Fomu uliisoma kabla ya kusaini
Shahidi: Ndio
Wakili: Unakumbuka nani aliyeona na kusoma namba za bastola
Shahidi: Afande Jumanne
Wakili: Katika maelezo yako hakuna mahali popote umesema uliposoma namba za bastola na kujiridhisha
Shahidi: Kwenye kuandika haijaandikwa lakini nimesema
Wakili Kibatala: Kwenye maelezo yako kuna sehemu umetaja jina la bastola
Shahidi: Kwenye maelezo hayapo
Wakili: Hii fomu aliijaza nani
Shahidi: Afande Jumanne
Wakili: Unajua bastola inatambulishwa kwa jina ndio uende kwenye namba
Shahaidi: Sifahamu
Wakili: Katika kielelezo cha bastola kuna mahali pana ufafanuzi wa namba CZ100
Shahidi: Hakuna
Wakili: Uliongozwa kufafanua chochote kuhusu hayo namba
Wakil: Kwenye laini ya Voda hukutolea ufafanuzi wowote kuhusu ICD namba.
Shahidi: Hapana
Wakili: Kuna mahali popote umemzungumzia Ramadhani Kingai
Shahidi: Hapana
Wakili: Kuna mahali umemzungumzia ulimsikia Ramadhani Kingai akijitambulisha kwa washtakiwa
Shahidi: Sijasema
Wakili: Afande Jumanne yeye wakati anajaza alikuwa amesima
Shahidi: Ndio
Wakili: Na huu mwandiko nadhifu uliandikwa akiwa amesimama
Shahidi: Ndio
Wakili: Kuna sehemu umemzungumzia grosari kati maelezo yako
Shahidi: Hakuna ni baa
Wakili: Kuna mahali popote umefafanua
Shahidi: Sijafafanua
Wakili: Duka lako la mbege liko mbali fremu ndio ziko karibu
Shahidi: Ndio
Wakili: Kutoka kwenye duka na fremu nyingine na mahali watuhumiwa waliokamatwa pana umbali gani.
Shahidi: Kama hatua tatu
Wakili: Wakati wanakamatwa je fremu zote zilikuwa wazi
Shahidi: Zilikuwa wazi
Wakili: Wakiacha watu kwenye hizo fremu wakakufuata
Shahidi: Ndio
Wakili: Unasema umeishi huko kwa miaka nane
Shahidi: Hilo eneo ni la Kiongozi wa Serikali ya mtaa
Wakili: Mwambie Jaji anaitwa nani
Shahidi: Maeleo
Wakili: Ukiacha huyo Kiongozi mwambie Mheshimiwa Jaji kama kuna kiongozi mwingine
Shahidi: Yupo
Wakili: Ulitoa ufafanuzi kuhusiana na muda uliokuwa unaenda saluni kuosha nywele ulikaa muda gani
Shahidi: Robo saa
Wakili: Ukarudi kufanya usafi ulitumiwa muda gani
Sahahid: Robo saa
Wakili: Kisha ukaka njee ya fremu yako
Wakili: Si unaona kuna tatizo la muda
Shahidi: Ndio
Wakili: Na hujalitolea ufafanuzi
Shahidi: Ndio
Wakili: Unataka nani alitatue
Shahidi: Mimi mwenyewe
Wakili: Hawa washtakiwa wawili walipigwa pingu uliemwambia nini kilitokea
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulimwambia Jaji mlienda central
Shahidi: Ndio
Wakili: Ulimwambia kwenye gari kuna maafisa wa polisi mlipanda nao
Shahidi: Ndio
Wakili: Waliwahi kuwaambia hii kesi imefunguliwa Dar es Salaam
Shahidi: Hapana
Wakili: Uliwahi kusikia ofisa yoyote wakimuhoji Moses Linenje
Shahidi: Nilisikia wakimuhoji mwenzenu
Wakili: Katika maelezo yako ulimzungumzia
Shahidi: Nilimzungumzia huko mwanzo
Wakili: Kuna mahali ulimzungumzia watatu
Shahidi: Hapana wawili
Wakili: Huyu wa tatu umemzungumzia leo
Shahidi: Ndio
Wakili: Hakuna mahali popote umemzungumzia katika maelezo yako kijana aliyekuwa anasajili smu.
Wakili: Uliona wakiwa wanasajili
Shahadi: Ndio
Shahadi: Mweleze Jaji walikuwa wanasajili laini gani
Shahadi: Sijui
Wakili: Mlivyofika central polisi mwambie Jaji kama ulishuhudi vile vifaa vikiingizwa kwenye daftari la polisi
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulimwambia Jaji iwapo umezungumzia vitu vingine walivyopatikana navyo ikiwemo waleti
Shahidi: Sijazungumzia
Wakili: Kama ulishudia mali za washtakiwa zikiingizwa kwenye kitabu
Shahidi: Sijasema
Wakili: Sema dada Ester ulimzungumzia umefafanua
Shahidi: Hapana
Wakili: Unafahamu vitambulisho vya wamachinga
Shahidi: Ndio
Wakili: Ili tuamini unaishi eneo umemzungumzia kama hicho unacho
Shahidi: Hapana
Wakili: Hata kumwambia kibanda hakina jina
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulimwambia Jaji mshtakiwa Mohamed alikuwa amevaa nguo za namna gani
Shahidi: Sikusema
Wakili: Umesema kielelezo ID kilijazwa eneo la tukio
Shahidi: Hapana
Shahidi: Ulisema kama zile nakala zilijzwa tatu na moja akapewa mshtakiwa.
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulimweleza Jaji kuwa maelezo yako yaliandikwa na wakili anayeitwa Francis,
Shahidi: Hapana
Wakili: Umesema bastola ina rangi nyeusi kataika maelezo yako kuna mahali ulipotaja
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulitoa ufafanuzi wa muda mliotumia njiani kutoka Rau hadi Moshi central
Shahidi: Hapana
Wakili: Ulifafanua muda mliotumia kituo cha polisi central
Shahidi: Hapana
Wakili: Uliwahi kusema kama central ulikuwa unapafahamu kabla ya hiyo siku
Shahidi: Hapana
Wakili: Baada ya kupatikana kwa dawa za kule ya mweleze Jaji ni nini kilifanyika
Shahidi: Hapana
Wakili: Mweleze Jaji kama kuna sehemu ulimzungumzia hatma ya haya madawa ya kulevya
Shahidi: Sijazungumza
Wakili: Mheshimiwa Jaji kwa shahidi huyu naomba kuishia hapa.
Wakili: Mweleze Jaji kama kuna sehemu ulimzungumzia hatma ya haya madawa ya kulevya
Shahidi: Sijazungumza
Wakili: Mheshimiwa Jaji kwa shahidi huyo naomba kuishia hapa
Upande wa utetezi umemaliza kumuhoji shahidi
Wakili wa Serikali, Ester Martin anasimamia na kumuhoji shahidi
Wakili Easter: Uliulizwa na wakili Mallya ni rangi gani uliona katika nguo aliyovaa mshtakiwa.
Shahidi: Niliona rangi nyeupe kijani na nyeusi
Wakili: Uliulizwa maelezo uliyotoa polisi na uliyotoa mahakamani kuna baadhi hayapo ikiwemo muda wa kufanya usafi na wakati watuhumiwa wanakamatwa je unaweza kuifafanulia mahakama ni kwanini hayo yametokea
Shahidi: Hayo yamejitokeza kwa kuwa ni maandishi tu yale niliyoandika na kutoa hapa mahakani
Wakili Kidando: Hebu tufafanulie ulichokiona kuhusiana na kusajili laini
Sahahid: Niliona wakiwa na kijana anaessajili laini
Wakili Kidando: Katika maelezo yako ulisema uliona vijana wawili na hapa mahakamani ukasema ni watatu hebu fafanua ni wapi ulipoona wawili
Shahidi: Wakati wa ukamataji
Wakili: Hebu tueleze ni lini umelifahamu jina la Adamoo
Shahidi: Nimeelifahamau leo
Wakili Kidando: Uliulizwa swali kuhusiana na hati ya utambuzi kuhusiana na CZ100 hebu tueleze unamfahamu nini kuhusiana na kilichaoandikwa
Sahahidi: Nafahamu namba A5340
Wakili: Umeulizwa swali kuhusiana na maelezo yako kuhusu baa na grosari washtakiwa walikuwa wapi
Shahidi: Walikuwa kwenye Grosari ya dada Ester
Wakili: Uliulizwa swali la wewe muda ulifika eneo lako la biashara kuhusu kufika eneo lako la kufanya usafi kwenda saluni hebu ifafanulie Mahakama ilikuwa muda gani
Sahahid: Saa saba mchana
Wakili: Uliulizwa baada ya washtakiwa kufikishwa polisi kama malai zao ziliandikwa hebu iambie Mahakama.
Shahidi: Sikusema kwa kuwa sijaulizwa
Wakili: Uliulizwa kuhusu kuwepo kwa jina la mtu anaitwa Kingai wakati wa ukamataji ni nani alikuwepo siku ya ukamataji
Shahidi: Sikuzungumza kwa sababu sikujua ni askari gani aliyekamata
Wakili: Mheshimiwa kwa leo tunakomea hapo
Jaji: Shahidi tunakushukuru unaweza kwenda
Wakili: Kidando Mheshimiwa Jaji tunaomba ahirisho hadi kesho saa 3:30 tutakapoendelea na shahidi mwingine.
Kibatala: Hatuna pingamizi Mheshimiwa Jaji
Jaji: Maombi ya kuahirishwa yanakubaliwa upande wa mashitaka mlete shahidi na washtakiwa wataendelea kuwa chini ya Magereza.
Advertisement
0 maoni:
Chapisha Maoni
ANDIKA MAONI YAKO HAPA